KUFANYIKA KWA KIKAO CHA BARAZA LA SHULE FEBRUARI 2024

 


MKUU WA SHULE AKIFUNGUA NA KUANZA KUJIBU HOJA ZA WANAFUNZI





Uongozi wa shule ya sekondari uchile umefanya kikao cha baraza la walimu na wanafunzi tarehe 14 februari 2024 ikiwa ni kujadili changamoto na kujibu hoja zilizo tokana na vikao vya madarasa ambapo mkuu wa shule Neusta Antony Nyandwi amejibu hoja mbalimbali zilizo jitokeza katika vikao na baraza hilo ikiwa ni kuthamini na mkakati wa kuondoa changamoto wanazo pitia wanafunzi katika kujifunza. walimu wote wa shule ya sekondari walihusika katika kikao hicho wakijibu hoja mbalimbali ambazo wanafunzi walizitoa katika vikao vyao na baraza hilo.
Kwa ujumla kikao kiliisha vizuri, ambapo wanafunzi walisema yanayo warudisha nyuma katika ujifunzaji wao na uongozi wa shule kuahidi kutatua yale yaliyo ndani  ya uweo wao na mengine kufikisha katika ngazi za juu kwa msaada.
Mkuu wa shule anathamini demokrasia kwa mwanafunzi na mwalimu wa shule ya sekondari uchile kwani ni nyenzo muhimu katika elimu.

FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA UCHILE SEKONDARI MWAKA 2024

 Pakuwa FOMU ya kijiunga kidato Cha kwanza MWAKA 2024 uchile sekondari soma na pitia maelezo muhimu yaliyo tolewa na taasisi.



MATOKEO YA MWISHO WA MWAKA KWA KIDATO CHA TATU 2023 YAMETOLEWA

 


HABARI: 

NDUGU MZAZI/ MLEZI WA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU UCHILE SEKONDARI. TUNAPENDA KUKUTAARIFU KUWA MATOKEO YA MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA (JOINT ANNUAL EXAMINATION )  YAMETOKA LEO TAREHE 11/ 12 2023. TAZAMA NA PAKUA  MATOKEO HAYO KUPITIA TOVUTI TEMBELEA UKURASA WETU WA MATOKEO.

MAAGIZO;

WANAFUNZI WOTE KIDATO CHA NNE MWAKA 2024 UCHILE SEKONDARI WANATAKIWA

1. KUKAA SHULENI

2. WAJE NA MCHANGO WA CHAKULA 

i. Mahindi debe 9 kwa mwaka au debe 5 kwa nusu muhula

ii. Maharage debe 3 kwa mwaka   au  debe 1  na nusu kwa nusu muhula

iii. Fedha Tsh 80000/= kwa mwaka au  Tsh. 40000/= kwa nusu muhula

3. Rim 2 

NB: SHULE ITAFUNGULIWA TAREHE 8/1/2024

FUATILIA MAENDELEO YA MWANAFUNZI KUPITIA TOVUTI YETU: ASANTE.

WASILIANA NASI KWA NAMBA

MKUU WA SHULE: 0755311154.

MAKAMU MKUU WA SHULE: 0763777991.

MTAALUMA: 0745006848.

TAARIFA KWA UMMA

Uongozi wa shule ya sekondari uchile unawataarifu wazazi na walezi wote wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka kidato cha tatu kuhudhuria kikao cha wazazi kitakacho fanyika Tarehe 8/12/2023 saa 9:00 asubuhi katika shule ya sekondari uchile.