KUFANYIKA KWA KIKAO CHA BARAZA LA SHULE FEBRUARI 2024

 


MKUU WA SHULE AKIFUNGUA NA KUANZA KUJIBU HOJA ZA WANAFUNZI





Uongozi wa shule ya sekondari uchile umefanya kikao cha baraza la walimu na wanafunzi tarehe 14 februari 2024 ikiwa ni kujadili changamoto na kujibu hoja zilizo tokana na vikao vya madarasa ambapo mkuu wa shule Neusta Antony Nyandwi amejibu hoja mbalimbali zilizo jitokeza katika vikao na baraza hilo ikiwa ni kuthamini na mkakati wa kuondoa changamoto wanazo pitia wanafunzi katika kujifunza. walimu wote wa shule ya sekondari walihusika katika kikao hicho wakijibu hoja mbalimbali ambazo wanafunzi walizitoa katika vikao vyao na baraza hilo.
Kwa ujumla kikao kiliisha vizuri, ambapo wanafunzi walisema yanayo warudisha nyuma katika ujifunzaji wao na uongozi wa shule kuahidi kutatua yale yaliyo ndani  ya uweo wao na mengine kufikisha katika ngazi za juu kwa msaada.
Mkuu wa shule anathamini demokrasia kwa mwanafunzi na mwalimu wa shule ya sekondari uchile kwani ni nyenzo muhimu katika elimu.

No comments: